MTAKIE NDUGUYAKO KHERI YA JUM'AA

Mapenzi ya Allah yawe maliwazo kwako, Akuruzuku imani na huba moyoni mwako, Pepo yake Rahmani iwe ndio makaazi yako, Akupe yalo mema kuzidi fikra zako. ***AMEEN*** Jum'a Kareem!!


Siku Tukufu imewadia, Yarraby tunusuru na Balaa za Duniya, Tufaulu Mitihani ya kilimwengu, Tuwe ni wenye kukumbuka na kushukuru Fadhla na Ukarimu wako. ****AMEEN!!!**** Jum'a Mubarak!!!

Rabbi tuvike libasi Leo na kesho Qiyama Tuondoshe wasi wasi Utwepushe zahma Tusitiri na maa'si Tusiwe wenye kuzama Awe mbali Iblisi Nasi peponi maqama, Amiyn **Jumaa Kareem**

Ewe khalikul' bashar, Muumba na muumbua, Tuepushe kulli sharr, Tuno na tusozijua, Utupe yalo sahal, Kwako tunategemea, Tufufue na Rasul, Peponi nayeye kuwa. Amiyn, Jumaa maqboor.

Leo nakuvisha koja tena lilo na thamani, Si viluwa si asumini ni subra koja la Muumini, Ilahi akuauni maovu akukhini, Mema akuzidishie akujazie kapuni. ****AMEEN!!!**** **JUMAA KAREEM**

Angalia utukufu wa Ijumaa: SubhanaAllah!! M/Mungu alimuumba Adam siku ya Ijumaa, Ijumaa Adam akaletwa duniani, Ijumaa Adam akafariki, Ijumaa ukiomba Dua inakubaliwa, Qiyama kitasimama Ijumaa. Jee yendapo Ijumaa ya leo itakuwa Qiyama Umejiandaa vp?? **Jum'aa Kareem**

Rabbi akupe Taufiq Nuru kukuangazia, Azikunjuwe riziki mambo kukunyoshea, Upatacho kibariki kitoshe na kubakia, Usikutane na dhiki ya Akhera na Dunia. ****AMEEN!!!**** **JUMAA KAREEM**

Nuru ya allah imulike kwako,ikutimizie mahitaji yako.riziki ya halali iwe pato lako,upendo uwe chakula chako,nyayo yako kuu iwe qur'an. Ijumaa karim.

Yuko wapi kama Wewe Mja ulo na Imani, Dua zitakabaliwe uombazo kwa Manani, Milango Ufunguliwe na Malaika Peponi, Haja utimiziwe ulonuia Moyoni. Ameen! J'maa/krm.

Amesema mtume wa Allah (s.a.w): ''ramadhani mpaka ramadhani,ijumaa mpaka ijumaa,swala mpaka swala ni vifutio vya madhambi zikiepukwa dhambi kubwa kubwa" tumuombe Allah kwa huruma zake ijumaa ya leo inshallah atufutie madhambi yetu tuliyofanya tukiwa tunajua au hatujui. IJUMAA KAREEM.

WWW.MSANGI.WEN.SU

BACK | EMAIL | TERMS

© 2007 ~ 2011